top of page

Dawa

ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.

 

Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.

Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Ranitidine

Ranitidine

Ranitidine ni dawa ambayo huzia tindikali isitengenezwe kutoka kwenye seli za ukuta wa tumbo. Dawa hii iliyopo kwenye kundi la dawa inayozuia risepta za histamine (H2), huzuia homoni ya histamine ambayo huchochea kutengenezwa kwa tindikali tumboni ili isishiriki katika kazi hiyo.

Nizatidine

Nizatidine

Nizatidine ni dawa ya kuzuia uzalishaji tindikali inayotumika katik amatibabu ya kucheua tindikali na maradhi mengine yanayotokana na uzalishaji wa tindikali.

Pioglitazone

Pioglitazone

Pioglitazone ni dawa ya kutibu kisukari aina ya pili iliyo kwenye kundi la thiazolidinedione.

Eplerenone

Eplerenone

Eplerenone ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu Iliyo kwenye kundi la dawa linaloitwa Potasiamu sparing diuretic. Dawa hii huwa maarufu kwa jina la Inspra

Risperidone

Risperidone

Risperidone ni dawa inayotumika kwenye matibabu ya magonjwa ya akili.

Pantoprazole

Pantoprazole

Ni dawa iliyo kundi la Protoni pumpu inhibita inayofanya kazi ya kuzuia uzalishaji wa tindikali tumboni.

Famotidine

Famotidine

Famotidine ni dawa ambayo huzia tindikali isizalishwe kutoka kwenye seli za ukuta wa tumbo zinazoitwa gastrini. Dawa hii iliyopo kwenye kundi la dawa zinazozuia H2 risepta antagonisti, huzuia kemikali ya histamine ambayo huchochea kutengenezwa kwa tindikali tumboni isishiriki katika kazi hiyo.

Omeprazole

Omeprazole

Omeprazole ni dawa iliyopo kwenye kundi la protoni pumpu inhibita ambayo hutumika kutibu magonjwa mbalimbali yanayotokana na kuzalishwa kwa wingi kwa tindikali za tumbo.

Lansoprazole

Lansoprazole

Lansoprazole ni dawa iliyopo kwenye kundi la proton pump inhibitors yenye uwezo wa kuzuia tindikali kutengenezwa tumboni na hivyo kuwa na uwezo wa kutumika kutibu hali mbalimbali zinanazo sababishwa na uzalishaji wa tindikali tumboni kama ugonjwa wa vidonda vya tumbo na kucheua tindikali.

Rabeprazole

Rabeprazole

Rabeprazole ni dawa ya kupunguza uzalishaji wa tindikali tumboni iliyo kwenye kundi la dawa za Protoni pampu inhibita.

Cimetidine

Cimetidine

Cimetidine ni dawa ambayo inazuia kutolewa kwa histamine na hivyo kuzuia kutengezwa kwa tindikali tumboni. Hivyo dawa hii hutumika kutibu matatizo mbalimbali yanayotokana na tindikali ya tumboni.

Esomeprazole

Esomeprazole

Ni dawa iliyopo kwenye kundi la proton pump inhibita ambayo huzuia uzalishaji wa tindikali kutoka kwenye ukuta wa seli za tumbo na hivyo kutibu hali mbalimbali ambazo husababishwa na tindikali ya tumboni kama vile vidonda vya tumbo na kiungulia.

Hujapata dawa unayotafuta?

 

Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa  "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

bottom of page