top of page

Dawa

ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.

 

Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.

Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Lurasidone

Lurasidone

Lurasidone ni dawa ya kutibu magonjwa ya akili na hali ya moyo wa mtu mfano magonjwa ya skizofrenia, dipresheni inayoambata na madhaifu ki baipola. Dawa hii ni kizazi kipya kwenye kundi la dawa liitwalo atipiko antisaikotiki.

Acarbose

Acarbose

Acarbose ni dawa inayotumika kushusha sukari kwenye damu kwa wagonjwa wa kisukari aina ya pili. Dawa hii hutumika kuzuia ongezeko la kiwango cha sukari kwenye damu mara baada ya kula.

Repaglinide

Repaglinide

Repaglinide ni dawa ya inayotumika katika matibabu ya kisukari aina ya pili, iliyo kundi la meglitinide.

Nateglinide

Nateglinide

Nateglinide ni dawa inayotumika kushusha kiwango cha sukari katika damu kwa wagonjwa wenye kisukari aina ya pili. Dawa hii ipo kwenye kundi la dawa linaloitwa meglitinide, hufanya kazi kwa haraka na ndani ya muda mfupi.

Azathioprine

Azathioprine

Azathioprine ni dawa jamii ya imyunosaprizanti inayofanya kazi ya kupunguza mwitikio wa mfumo wa kinga dhidi ya maradhi. Dawa hii hutumika pamoja na dawa zingine ili kuzuia mwili kukataa figo ya kupandikiza ili ifanye kazi vizuri.

Tolazamide

Tolazamide

Tolazamide ni dawa inayotumika katika matibabu ya kisukari na Ipo kwenye kundi la kizazi cha kwanza cha dawa za sulfonylurea.

Glimepiride

Glimepiride

Glimepiride ni dawa inayotumika kwenye matibabu ya wagonjwa wa kisukari aina ya pili. Dawa hii inanguvu zaidi ya kushusha kiwango cha sukari kwenye damu na kufanya kazi kwa muda mefu zaid na ipo katika kundi la kizazi cha tatu cha dawa jamii ya sulfonylurea.

Glicazide

Glicazide

Glicazide ni dawa mojawapo iliyo kwenye kundi la sulfonylurea inayotumika kushusha kiwango cha sukari ya damu kwa wagonjwa wa sukari.

Acetohexamide

Acetohexamide

Acetohexamide ni dawa iliyopo kwenye kundi la sulphonylurea inayotumika kutibu ugonjwa wa kisukari aina ya pili.

Exenatide

Exenatide

Exenatide ni dawa inayotumika kwenye matibabu ya kisukari aina ya pili iliyo kwenye kundi la dawa linalojulikana kama Glucagon like peptide 1 Agonisti. Dawa hii iliyo maarufu kwa jina la Byetta hupatikana kwakwenye mfumo wa maji na hutumika kwa kuchoma sindano chini kidogo ya Ngozi.

Dulaglutide

Dulaglutide

Dulaglutide ni dawa inayotumika kwenye matibabu ya kisukari aina ya pili iliyo kwenye kundi la dawa linalojulikana kama Glucagon like peptide 1 Agonisti. Dawa hii iliyo maarufu kwa jina la Trulicity hupatikana kwakwenye mfumo wa maji na hutumika kwa kuchoma sindano chini kidogo ya Ngozi.

Metolazone

Metolazone

Metolazone ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu Pamoja na kupunguza uvimbe wa mwili kutokana magonjwa mbalimbali kama kuferi kufanya kazi kwa moyo na figo na pia inaweza kuzuia shida ya kupumua kutokana na maji kujaa kwenye mapafu.

Hujapata dawa unayotafuta?

 

Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa  "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

bottom of page