top of page

Dawa

ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.

 

Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.

Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Amoxyclav

Amoxyclav

Amoxyclav ni dawa ya antibayotiki yenye mchanganyiko wa Amoxicillin na Clavunic acid, dawa hi hujulikana kwa jina jingine la amoxiclav, aphaclav. Hutumika kutibu maambukizi mbalimbali ya Bakteria mwilini.

Dolutegravir

Dolutegravir

Dawa hii huuzwa katika kwa jina la Tivicay, Dolutegravir ni aina ya dawa mojawapo za kudhibiti maambukizi ya VVU. Dawa hii hutumika ikiwa imeungana na dawa zingine za kudhibiti maambukizi ya VVU-ARTs

Tenofovir

Tenofovir

Dawa hii huuzwa katika jina la Viread na hutumika ikiwa imeungana pamoja na dawa zingine za kuthibiti makali ya VVU HIV (ART)

Atazanavir

Atazanavir

Atazanavir ni dawa mojawapo ya kudhoofisha makali ya Virusi vya UKIMWI (ART) na ipo kwenye kundi la dawa zinazoitwa Proteaz inhibita- PIs

Truvada

Truvada

Truvada ni dawa mojawapo ya kudhoofisha makali ya Virusi vya UKIMWI (ART) na ni muunganiko wa dawa mbili zilizo kwenye makundi ya NRTIs na NtRTIs

Zidovudine (AZT)

Zidovudine (AZT)

Zidovudine ni dawa mojawapo ya kudhoofisha makali ya Virusi vya UKIMWI(ART) na ipo kwenye kundi la dawa zinazoitwa NRTIs.

Emtricitabine (FTC)

Emtricitabine (FTC)

Emtricitabine (FTC) ni dawa mojawapo ya kudhoofisha makali ya Virusi vya UKIMWI (ART) na ipo kwenye kundi la dawa zinazoitwa NRTIs.

Abacavir (ABC)

Abacavir (ABC)

Abacavir ni dawa mojawapo ya kudhoofisha makali ya Virusi vya UKIMWI(ART) na ipo kwenye kundi la dawa zinazoitwa NRTIs.

Aspirini

Aspirini

Aspirini ni dawa inayotumika kupunguza homa na maumivu kiasi na wastani yanayotokana na maumivu ya misuli, maumivu ya jino na homa baridi. Dawa hii pia inaweza kupunguza maumivu ya athraitizi.

Paracetamol

Paracetamol

Parasetamo kwa jina lingine hujulikana kama acetaminofeni ni dawa inayotumika kutuliza homa pamoja na maumivu.

Kalisiamu

Kalisiamu

Kalisiamu ni madini yanayopatikana katika vyakula vingi. Hiki ni kirutubisho ambavyo viumbe hai vyote vinahitaji ikiwa pamoja na wanadamu. Madini haya huwa na nguvu na umuhimu kwa afya ya mfupa.

Loperamide

Loperamide

Ni dawa iliyo kwenye kundi la dawa zinazozuia kuhara. Dawa hii inaweza kupatikana kwa majina tofauti kulingana na kiwanda kilichotengeneza lakini kiini cha dawa ni kimoja ambacho ni loperamide. Jina jingine la dawa hii ni Imodium

Hujapata dawa unayotafuta?

 

Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa  "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

bottom of page