top of page

Dawa

ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.

 

Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.

Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Dawa Ciprofloxacin

Dawa Ciprofloxacin

Ciprofloxacin ni moja kati ya antibiotiki kwenye kundi la Fluoroquinolones yenye uwezo wa kukabiliana sana na bakteria jamii ya gramu hasi. Majina mengine ya dawa hii ni etraxal, Ciloxan, Cipro, Cipro HC, Ciprodex, Otiprio, Otixal, Otovel na Proquin

Dawa Ceftriaxone

Dawa Ceftriaxone

Ceftriaxone ni moja ya antibiotiki ya kizazi cha tatu cha kundi la Cephalosporins yenye wigo mpana wa kuua vimelea aina ya Aerobic na Anaerobic, gramu hasi na gramu chanya . Majina mengine ya dawa hii ni Rocephin

Ampicillin

Ampicillin

Ni dawa jamii ya antibayotiki iliyo kwenye kundi la Penicillin. Dawa hii ni maarufu kwa majina mengine kama Ampi, Omnipen, Penglobe na Principen.

Secnidazole

Secnidazole

Secnidazole ni dawa ya antibayotoki kudi la nitroimidazole inayotumika kutibu maambukizi yanayosababishwa na bakteria.

ALU

ALU

ALU ni dawa yenye maana ya artemether/lumefantrine, mchanganyiko wa dawa mbili ya artemether na lumefantrine iliyo kwenye kundi la dawa za kutibu malaria.

Misoprostol

Misoprostol

Misoprostol dawa aina ya prostaglandin, dawa hii huwekwa kwenye makundi mbalimbali ya dawa kutokana na uwezo wake wa kutibu hali na magonjwa mbalimbali.

Levonorgestrel

Levonorgestrel

Levonorgestrel ni dawa mojawapo iliyo kwenye kundi la dawa za progestin, hutumika kama dawa za uzazi wa mpango wa dharura. Dawa hii huzuia kutungishwa kwa mimba kwa kuzia ovari kutoa yai.

Nifedipine

Nifedipine

Nifedipine ni dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu pamoja na kuzuia tatizo la anjaina.

Dawa Isoniazid

Dawa Isoniazid

Isoniazid ni miongoni mwa dawa zinazotumika katika matibabu na kinga ya maambukizi ya kifua kikuu (TB), dawa hii ipo

Dawa Rifapentine

Dawa Rifapentine

Ni dawa ya antibiotic jamii ya macrolactams, inayotumika katika matibabu ya TB, dawa hii huzuia kimeng’enya polymerase kufanya kazi katika utengenezaji wa DNA ya baadhi ya seli isipokuwa seli za wanyama. Dawa hii huwa maarufu kwa jina jingine la priftin

Dawa ya Mebeverine

Dawa ya Mebeverine

Mebeverine ni dawa iliyo kwenye kundi la antispasmodic, dawa ambazo hufanya kazi ya kuzuia mijongeo ya misuli laini mwilini inayopeleka kutokea kwa change la tumbo. Dawa hii huwa na kazi ya kuondoa na kuzuia maumivu ya tumbo kutokana na tumbo kunyonga.

Dawa ya Nitrofurantoin

Dawa ya Nitrofurantoin

Ni dawa mojawapo ya kutibu maambukizi ya bakteria na hutumika sana kwa wajawazito kutibu UTI isiyo sugu kwa kuwa imeonekana haina madhara.

Hujapata dawa unayotafuta?

 

Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa  "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

bottom of page