top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, MD

30 Oktoba 2026, 12:50:58

shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.
Kinyesi chenye harufu mbaya

Kinyesi chenye harufu mbaya

Maelezo ya jumla


Harufu ya kinyesi hutokana na bakteria wa utumbo wanaomeng'enya mabaki ya chakula. Ni kawaida kuwa na harufu isiyopendeza; harufu hubadilika kulingana na ulichokula.


Tatizo ni harufu mpya, kali kupita kawaida, inayoendelea, au inayoambatana na kuharisha, mafuta kwenye kinyesi, maumivu au kupungua uzito.


Aina na jinsi inavyojitokeza


  • Baada ya chakula fulani, kwa siku 1 hadi 2 – mayai, nyama nyingi, vitunguu, kabichi, vyakula vya viungo.

  • Pamoja na kuharisha cha ghafla – maambukizi ya utumbo.

  • Kinyesi cha mafuta, kinachong'aa, kinachoelea na vigumu kuflashi – chakula hakifyonzwi vizuri.

  • Kuharisha kwa harufu ya mayai yaliyooza, gesi nyingi na tumbo kujaa – giardia.

  • Harufu ya damu, kinyesi cheusi – soma Kuharisha kinyesi cheusi.


Visababishi


Chakula na dawa


  • Nyama nyingi, mayai, vitunguu, kabichi, pombe.

  • Kushindwa kumeng'enya laktosi ya maziwa.

  • Antibiotiki – hubadilisha bakteria wa utumbo.

  • Vidonge vya vitamini na madini kwa wingi.


Maambukizi


  • Giardia.

  • Amiba.

  • Salmonella na bakteria wengine wa sumu ya chakula.

  • Minyoo.

  • Kuharisha kwa bakteria C. difficile baada ya antibiotiki.


Chakula kutofyonzwa (malabsorption)



Mengineyo



Dalili zinazoambatana


  • Kuharisha.

  • Gesi na tumbo kujaa.

  • Maumivu ya tumbo.

  • Kinyesi cha mafuta kinachoelea.

  • Kupungua uzito – chakula hakifyonzwi.

  • Homa – maambukizi.

  • Uchovu na weupe – upungufu wa damu.


Dalili za hatari


Onana na daktari mapema ukiwa na harufu mbaya ya kinyesi pamoja na:


  • Damu kwenye kinyesi au kinyesi cheusi.

  • Kuharisha kwa zaidi ya siku 3 hadi 5, au dalili za upungufu wa maji.

  • Homa kali.

  • Kinyesi cha mafuta pamoja na kupungua uzito.

  • Kuharisha kwa muda mrefu ukiwa na VVU.

  • Kuharisha kuliko anza wakati au baada ya antibiotiki.


Vipimo


  • Kipimo cha kinyesi – vimelea (giardia, amiba, minyoo), bakteria, damu iliyojificha, mafuta.

  • Kipimo kamili cha damu.

  • Kipimo cha VVU – kwa kuharisha kwa muda mrefu.

  • Vipimo vya ini na kongosho; ultrasound.

  • Endoskopia au kolonoskopia – kwa dalili za muda mrefu.


Matibabu na huduma ya nyumbani


  • Kutokana na chakula – punguza vyakula vinavyokuletea harufu; kula mlo kamili.

  • Maambukizi – dawa kulingana na kimelea kilichopatikana; ORS na maji kwa kuharisha.

  • Kutomeng'enya laktosi – punguza maziwa; jaribu mtindi.

  • Chakula kutofyonzwa – kutibu chanzo (kongosho, nyongo, celiac); vimeng'enya vya kongosho kwa wanaohitaji.

  • Usitumie antibiotiki bila kipimo – zinaweza kuzidisha tatizo.


Kinga


  • Nawa mikono kwa sabuni kabla ya kula na baada ya choo.

  • Kunywa maji safi yaliyochemshwa au kutibiwa.

  • Kula chakula kilichopikwa vizuri.

  • Punguza pombe.

  • Tumia antibiotiki kwa ushauri tu.


Lini umwone daktari


  • Harufu mbaya ya kinyesi kwa zaidi ya wiki 1 hadi 2.

  • Mabadiliko ya choo yanayodumu.

  • Kinyesi cha mafuta kinachojirudia.

  • Gesi na tumbo kujaa vinavyoendelea.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Kinyesi changu kinanuka sana kuliko kawaida, ni nini?

Mara nyingi ni chakula ulichokula au maambukizi ya utumbo. Kama inaambatana na kuharisha, maumivu au homa, au inaendelea zaidi ya wiki, fanya kipimo cha kinyesi.

2. Kinyesi kinaelea na ni cha mafuta, kinanuka sana, ni nini?

Hii ni ishara kwamba mafuta hayafyonzwi vizuri – kongosho, nyongo, ini au ugonjwa wa utumbo. Onana na daktari, hasa kama unapungua uzito.

3. Naharisha kinyesi chenye harufu ya mayai yaliyooza na gesi nyingi, ni nini?

Dalili hizi mara nyingi zinaashiria giardia, kimelea kinachoenezwa kwa maji machafu. Kipimo cha kinyesi kitathibitisha na dawa zinapatikana.

4. Tangu nianze antibiotiki kinyesi kinanuka na naharisha, kwa nini?

Antibiotiki hubadilisha bakteria wa utumbo. Kwa wengi huisha baada ya kumaliza dawa. Kuharisha kwingi, damu au homa wakati wa antibiotiki kunahitaji daktari.

5. Nikinywa maziwa kinyesi kinanuka na naharisha, ni nini?

Huenda mwili haumeng'enyi laktosi. Punguza maziwa freshi au tumia mtindi.

6. Kinyesi kinanuka na kina kamasi, ni nini?

Kamasi pamoja na harufu mbaya inaweza kutokana na maambukizi kama amiba, utumbo nyeti au uvimbe wa utumbo mpana. Kama kuna damu au maumivu, fanya kipimo cha kinyesi.

7. Kinyesi kinanuka harufu ya damu na ni cheusi, ni hatari?

Ndiyo, inaweza kuwa damu kutoka tumboni. Nenda hospitali mara moja. Soma Kuharisha kinyesi cheusi.

8. Ninaharisha muda mrefu na kinyesi kinanuka, naweza kuwa na VVU?

Kuharisha kwa muda mrefu ni dalili inayoweza kuonekana kwa VVU isiyotibiwa, lakini ina visababishi vingi. Kupima VVU ni sehemu ya uchunguzi wa kawaida wa kuharisha kwa muda mrefu.

9. Kinyesi kinanuka sana baada ya kula nyama nyingi, ni tatizo?

Hapana, ni kawaida. Protini nyingi huacha mabaki yanayomeng'enywa na bakteria na kutoa harufu kali zaidi. Kula mboga na nyuzinyuzi husaidia.

10. Nifanye nini kupunguza harufu mbaya ya kinyesi?

Kula mlo kamili wenye mboga na nyuzinyuzi, kunywa maji ya kutosha, punguza pombe na vyakula vinavyokuletea harufu, na tibu maambukizi yoyote yaliyopatikana kwenye kipimo cha kinyesi.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeandikwa:

30 Oktoba 2026, 12:50:17

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada hii:

  1. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

  2. Merck Manual Consumer Version. Constipation in adults; Black stools; Malabsorption. Merck & Co.; 2024.

  3. World Health Organization. Diarrhoeal disease – fact sheet. Geneva: WHO; 2024.

bottom of page