top of page

Dawa

ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.

 

Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.

Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Dawa Moxifloxacin

Dawa Moxifloxacin

Moxifloxacin ni anitbayotiki ya jamii ya fluoroquinolone inayotumika kutibu maambukizi ya bakteria wanaodhuruwa na dawa hii kama maambukizi kwenye sainazi, njia za hewa na mapafu.

Dawa Levofloxacin

Dawa Levofloxacin

Levofloxacin ni moja ya antibayotiki jamii ya fluoroquinolone inayotumika kutibu maambukizi ya bakteria wanaodhuriwa na dawa kwenye njia ya hewa, ngozi, mfumo wa mkojo, tezi dume na waliojianika kwenye kimeta na plague.

Dawa Cefepime

Dawa Cefepime

Cefepime ni antibiotiki ya kizazi cha nne cha cephalosporin inayotumika katika matibabu ya magonjwa yanayosababiswha na maambukizi ya bakteria mbalimbali wanaodhuriwa na dawa hii kwenye mapafu, mfumo wa mkojo, via vya uzazi, nogzi n.k.

Dawa Imipenem

Dawa Imipenem

Imipenem ni moja kati ya antibiotiki jamii ya carbapenems yenye uwanja mpana wa kudhuru bakteria inayotumika sana ikiwa imeunganika na cilastatin ili kuongeza muda wa ufanyaji kazi wake na kuzuia madhara yake kwenye figo.

Dawa Imipenem/cilastatin

Dawa Imipenem/cilastatin

Imipenem/cilastatin ni moja ya antibiotic jamii ya Carbapenem iliyounganishwa na cilastatin, dawa hii hutumika kutibu magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na maambukizi ya bakteria wanaodhuriwa na dawa hii.

Dawa Artesunate

Dawa Artesunate

Artesunate ni dawa iliyo kwenye kundi la dawa za kutibu malaria kali, inayofahamika kwa jina jingine la Camequin

Dawa Cefpodoxime

Dawa Cefpodoxime

Cefpodoxime ni antibiotiki ya kizazi cha tatu cha cephalosporin inayotumika kutibu magonjwa yatokanayo na bakteria wa gram hasi na gram chanya.

Dawa Fosfomycin

Dawa Fosfomycin

Fosfomycin ni moja kati ya antibiotic inayotumika kuzuia ukuaji na kuua bakteria wanaosababisha maambukizi kwenye kibofu cha mkojo.

Dawa Aztreonam

Dawa Aztreonam

Aztreonam ni moja kati ya antibiotic jamii ya Monobactam inayotumika kutibu maambukizi ya bakteria gram hasi kama vile pseudomonas aeruginosa.

Dawa Pyrimethamine

Dawa Pyrimethamine

Pyrimethamine ni moja kati ya dawa inayotumika kutibu maambukizi yanayosababishwa na vimelea vya toxoplasma na malaria ambayo huingia kwenye ubongo na macho pia kukinga dhidi ya ugonjwa wa toxoplasmosis kwa watu wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Dawa Flibanserin

Dawa Flibanserin

Flibanserin ni dawa jamii ya Serotonin 5-HT-risepta agonist, inayotutumika kwa wanawake ambao hawajaingia komahedhi kutibu madhaifu yenye ya kupungua kwa hisia za kingono kwa ujumla yanayoambatana na masumbufu binafsi au ya mahusiano.

Dawa Primaquine

Dawa Primaquine

Primaquine ni dawa kunywa jamii ya aminoquinoline inayotumika katika matibabu ya malaria inayosababishwa na plasmodium vivax na ovale, pia hutumika kaa kinga ya malaria kwa watu wanaorejea nyumbani katika maeneo ambayo hayana malaria.

Hujapata dawa unayotafuta?

 

Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa  "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

bottom of page