Dawa
ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.
Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.
Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Dawa Piperacillin/tazobactam
Piperacillin tazobactam ni dawa ya antibayotiki katika kundi la penicillin iliyounganishwa na tazobactam kwa ajili ya kuongeza uwezo wake wa kutibu magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na bakteria haswa wa gramu hasi, na kiasi cha bakteria wa gramu chanya na anaerobiki. Tazobactam inayoongezwa kwenye dawa hii huwa na uwezo wa kuzuia kimeng’enya muhimu cha bakteria chenye jina la β-lactamase.
Hujapata dawa unayotafuta?
Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii











