top of page

Dawa

ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.

 

Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.

Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Telmisartan

Telmisartan

Telmisartan ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Angiotensini II risepta bloka (ARBs).Dawa hii huwa maarufu kwa jina la Micardis

Doxazosin

Doxazosin

Doxazosin ni aina ya dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa alfa bloka. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Cardura

Nicardipine

Nicardipine

Nicardipine ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa kalisiamu chaneli bloka.

Prednisolone

Prednisolone

Prednisolone ni dawa mojawapo kwenye kundi la glucorticoid inayofanana na cortisol. Hutumika kuzuia uvimbe kutokana na mwitikio wa kinga ya mwili, kudhorofisha kinga ya mwili, kuzuia saratani na kupunguza kipenyo cha mishipa ya damu.

Lixisenatide

Lixisenatide

Lixisenatide ni dawa mojawapo ya kutibu ugonjwa wa kisukari aina ya pili iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Glucagon like peptide 1 Agonisti.

Taspoglutide

Taspoglutide

Taspoglutide ni dawa mojawapo ya kutibu kisukari aina ya pili iliyo kwenye kundi la dawa linaloitwa Glucagon like peptide 1 Agonisti.

Semaglutide

Semaglutide

Semaglutide ni dawa mojawapo ya kutibu kisukari aina ya pili iliyo kwenye kundi la Glucagon like peptide 1 Agonisti.

Exenatide

Exenatide

Exenatide ni dawa mojawapo ya kutibu ugonjwa wa kisukari aina ya pili iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Glucagon like peptide 1 Agonisti. Dawa hii huwa maarafu pia kwa jina la Byetta.

Liraglutide

Liraglutide

Liraglutide ni dawa mojawapo ya kutibu ugonjwa wa kisukari aina ya pili iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Glucagon like peptide 1 Agonisti.

Nimodipine

Nimodipine

Nimodipine ni dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu pamoja na kuvia kwa damu kwenye uwazi wa sabuarakinoidi.

Gliquidone

Gliquidone

Gliquidone ni dawa mojawapo inayotumika kwenye matibabu ya ugonjwa wa kisukari iliyo kwenye kundi la sulfonylurea kizazi cha pili. Dawa hii inaweza kusababisha mgonjwa akakojoa mara kwa mara.

Timolol

Timolol

Timolol ni dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu kwenye mishipa ya damu na macho iliyo kwenye kundi la beta bloka.

Hujapata dawa unayotafuta?

 

Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa  "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

bottom of page