top of page

Dawa

ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.

 

Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.

Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Dapsone

Dapsone

Ni dawa iliyo kwenye kundi la dawa za kutibu ukoma- (antileprosi), dawa hii hutumika kwa pamoja na rifampicin na clofazimine ili kutibu ukoma.

Methotrexate

Methotrexate

Ni dawa ambayo ilikuwa ikijulikana kwa jina la amethopterin na huuzwa katika jina la Trexal, hufanya kazi kama dawa ya kushusha kinga za mwili.

Adalimumab

Adalimumab

Ni dawa kwenye kundi la saitokini moduleta, dawa zingine katika kundi hili ni, Infliximab na golimumab. Dawa hizi zimetengenezwa kutoka kwenye antibodi za monokrono, antibodi hizi hufanya kazi za kuzuia saitokani za inflamesheni na tyuma necrosis facta alfa. Dawa hii inatakiwa kutumika chini ya uangalizi maalumu kutoka kwa mtaalamu mbobezi wa dawa.

Golimumab

Golimumab

Ni dawa inayofanya kazi kwa kudhibiti kiamsha michomo mwilini chenye jina la tumor necrosis factor alfa.

Raltegravir

Raltegravir

Ramipril ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo katika kundi la dawa linaloitwa angiotensini konventing enzaimu inhibita- ACEIs. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Altace.

Lopinavir(LPV)/Ritonavir

Lopinavir(LPV)/Ritonavir

Lopinavir(LPV)/ritonavir ni dawa mojawapo ya kudhoofisha makali ya Virusi vya UKIMWI(ART) na Hepataitizi C, dawa hii ipo kwenye kundi la dawa zinazoitwa Proteaazi inhibita.

Rilpivirine

Rilpivirine

Rilpivirine ni dawa ya kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI iliyo kundi la NNRTIs.

Darunavir

Darunavir

Darunavir ni dawa mojawapo ya kudhoofisha makali ya Virusi vya UKIMWI(ART) na Hepataitizi C, dawa hii ipo kwenye kundi la dawa zinazoitwa Proteaazi inhibita.

Indomethacin

Indomethacin

Ni dawa jamii ya NSAIDs, hutumika kupunguza maumivu makali, kupunguza uvimbe kutokana na majeraha na kukakamaa kwa maungio ya mwili kutokana na ugonjwa wa athraitizi, gauti, bazaitizi na tendinaitizi inflamesheni

Amoxicillin

Amoxicillin

Ni antibiotiki inayotibu maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Kazi yake kuu kwa bakteria hawa ni kuua ama kuzuia ukuaji wao. Dawa hii huweza kutibu bakteria wa gramu hasina Gram chanya.

Clindamycin

Clindamycin

Ni antibiotiki iliyo kwenye kundi la lincosamide inayotumika kutibu maambukizi makali ya bakteria wanaouliwa na dawa hii pamoja na kutibu chunusi za vulgarizi. Kemikali ya lincosamide huvunwa kutoka kwa bakteria anayeitwa Streptomyces lincolnensis.

Folate

Folate

Ni aina ya vitamin B9 ambayo hupatikana kwenye vyakula. Madini haya huwa hayatengenezwi mwilini, hupatikana kwa kula vyakula vyenye Folate kwa wingi tu. Folate kabla ya kuingia kwenye damu, mfumo wa chakula huibadilisha na kuwa Vitamin B9

Hujapata dawa unayotafuta?

 

Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa  "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

bottom of page