top of page

Pata ujauzito wa mapacha| ULY CLINIC

Updated: Nov 12, 2020

Ufanye nini ili upate mimba ya mapacha

Tuanze kujibu swali hili kwa kufahamu kwanza namna gani mtoto hutengenezwa tumboniKufanyika kwa mtoto ndani ya tumbo la uzazi ni matokeo ya manii kuchavusha yai, kitendo hichi huitwa fetelaizesheni. Mara baada ya fetelaizeshen kilichotengenezwa huwa seli yenye sura ya mpira wenye muunganiko wa mbegu ya kiume na yai la mama, seli ndani ya mpira huu huanza kugawanyika na kutengeneza seli nyingi ambazo baadaye hufanya viungo mbalimbali vya mtoto katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito. Ili kuweza kutengeneza mapacha, inatakiwa mpira huu uliofanyika ujigawanye na mipila miwili au manii mbili tofauti zichavushe mayai mawili tofauti wakati wa fetelaizeshen. Vitendo hivi viwili hupelekea kuleta mapacha wa aina mbili yaani;

 • Mapacha wa kutofanana wanaojulikana kama mapacha wa daizaigotiki au frateno wanaotokea endapo manii mbili zimechavusha mayai mawili. Mapacha wa aina hii mara nyingi huwa hawafanani na huwa na vinasaba tofauti tofauti.

 • Mapacha wa kufanana- Hufanyika pale yai lililochavushwa na maniii kugawanyika na kutengeneza vijusi viwili katika kipindi cha wiki mbili za kwanza za ujauzito. Hutumia kondo moja la nyuma na hufanana vinasaba na jinsia na huitwa mapacha wa monozaigoti

Mambo yanayoongeza uwezekano mkubwa wa kupata mapacha;

 • Kuwa na historia ya ujauzito nyingi zilizotangulia

 • Kuwa mwanamke unayetoka kwenye familia yenye mapacha

 • Mwanamke kuwa na umri wa zaidi ya miaka 30. Katika umri huu mwanamke huzalisha homoni chochezi ya foliko kwa wingi na ksuababisha uwezekano wa kutoa mayai mawili kwa wakati mmoja.

 • Asili ya mtu- wanawake wenye asili ya bara la afrika na amerika wanahatari kubwa ya kupata mapacha kuliko wenye asili nyingine

 • Urefu- mwanamke mwenye urefu zaidi ya sentimita 162 huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata mapacha kuliko wanawake walio chini ya urefu huu

 • Tiba ya uzazi- matumizi ya njia ya uzazi ya kuchavusha mayai kwenye chupa na kupandikiza kwenye kizazi huongeza hatari ya mwanamke kupata mapacha

Njia asilia za kukusababisha upate mapacha


Njia zifuatazo zimeonekana kwenye tafiti kuongeza hatari ya kupata mimba mapacha

 • Kupumzika kidogo kabla ya kupata ujauzito mwingine unaofuata haswa baada ya kufululiza mimba mbili zinazofuatana.

 • Kupata ujauzito wakati wa kunyonyesha- kipindi hiki homoni ya prolaktini hutolewa kwa wingi na huleta hatari ya kupata mimba mapacha

 • Kula vyakula vyenye mchanganyiko wa maziwa maziwa asilia- maziwa huwa na homoni nyingi za ukuaji ambazo huongeza hatari ya kupata mapacha

 • Kula vyakula vyenye protini kwa wingi- vyakula asilia vyenye protini kwa wingi kama maharagwe ya soya n.k huongeza hatari ya kupata mimba mapacha kwa kusababisha ovari kuzalisha mayai mengi zaidi

 • Mwenza wako kutumia madini ya zinki kwa wingi- madini haya huchochea uzalishaji wa manii kwa wingi hivyo ni vema mwenza wako akatumia pia ili kuzalisha manii za kutosha kuweza kutengeneza mapacha

 • Matumizi ya madini foliki asidi kwenye ujauzito- husaidia kupunguza uwezekano wa kupata watoto wenye shida kwenye mfumo wa fahamu kama tundu kwenye uti wa mgongo na kichwa maji. Inashauriwa kila mwanamke mjamzito kutumia madini haya

 • Tumia njia za uzazi za kupandikiza mayai yaliyochavushwa kama vile njia ya IVF au IAI

 • Matumizi ya dawa kama vile dawa za kuongeza uzalishajiwa mayai pergonal, clomid, humegon na zinginezo

 • Matumizi ya vyakula asilia kama mbegu za kitani, mihongo, mafuta ya primrose n.k

Hatari ya ujauzito mapacha kwa mama na mtoto ni;


Bonyeza kusoma makala zingine zaidi kuhusu;


Rejea za mada hii


 1. Obstetric by Ten teacher chapisho la 20 kurasa namba 225na226.

 2. Twins research Australia. Twins genetics. https://www.twins.org.au/research/twin-and-data-resource/76-types-of-twins. Imechukuliwa 08.11.2020

 3. National human genome research institute. Fraternal twins. https://www.genome.gov/genetics-glossary/Fraternal-Twins. Imechukuliwa 08.11.2020

 4. The tech interactive. Twins. https://genetics.thetech.org/ask-a-geneticist/twin-genetics. Imechukuliwa 08.11.2020

499 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page